Jeremiah 50:33-34

33 aHili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Watu wa Israeli wameonewa,
nao watu wa Yuda pia.
Wote waliowateka wamewashikilia sana,
wanakataa kuwaachia waende.

34 bLakini Mkombozi wao ana nguvu;
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.
Atatetea kwa nguvu shauri lao
ili alete raha katika nchi yao,
lakini ataleta msukosuko
kwa wale waishio Babeli.

Copyright information for SwhKC